Tarehe 19/04/202 Imeandaliwa na: PAUL MASAWE
SOMO LA KWANZA
A. MAANDIKO MATAKATIFU.
Utangulizi,
Ni nini maana ya Maandiko Matakatifu?
Maandiko Matakatifu ni ufunuo usiokosea wa mapenzi ya Mungu.
Agano la kale na Agano jipya ni Maandiko Matakatifu ya Mungu yaliyoandikwa, yaliyotolewa kwa kuvuviwa wanadamu watakatifu wa Mungu ambao walinena na kuandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Katika Neno hili, Mungu amewapatia wanadamu ujuzi muhimu kwa wokovu, ndicho kiwango cha tabia na kipimo cha uzoefu. Masomo : (2Pet.1:20-21; 2Tim.3:16-17; Zab.119:105; Mith.30:5-6; Isa.8:20; Yoh.17:17; 1Thes.2:13; Ebr.4:12).
1.0 UFUNUO WA MUNGU.
Wakati katika historia wako waliohoji kuwepo kwa Mungu, wako wengine walioshuhudia yupo na amejifunua mwenyewe. Ni jinsi gani amejifunua na joins gani Biblia inazungumzia kujifunua kwake?
1.1. UFUNUO WA KIUJUMLA
. Wazo juu ya tabia ya Mungu ambayo historia, tabia ya mwanadamu, dhamiri na uumbaji huitwa Ufunuo wa kiujumla kwa kuwa unapatika kwa owte na huvutia kwenye fikra. Kwa mamilioni ya Wanadamu ,mbingu zauhubiri utakufu wa Mungu na anga latangaza kazi ya mikono yake (Zab. 19:1). Mambo yake yasiyoonekana sasa yako Dhahiri na wanadamu hawana udhuru. (Rum.1:20). Wengine humuona mungu katika mahusiano kwa upendo wa kirafiki, kifamilia, mume na mke, wazazi kwa Watoto (Isa.66:13; Zab.103:13).
Hata hivyo jua laweza kuumiza nchi ikawa jangwa,mvua yaweza kuloeta mafuriko,ardhi yaweza kupata ufa,kuanguka na kuvunjika. Mahusiano ya wanadamu hujaa wivu,kijicho,hasira chuki n ahata kuleta maafa. Ulimwengu unaotuzunguka hutupatia ishara zinazoonesha na kuleta maswali mengi kuliko majibu. Huonesha pambano baina ya wema na uovu lakini havisemi kwa vipi na kwa nini pambano lilianza, nani anapigana kwa nini na ni nani ambaye hatimaye atashinda.
1.2. UFUNUO MAALUM.
Dhambi inaficha kujifunua kwa Mungu kupitia kazi yake ya umbaji kwa kuzuilia uwezo wetu kutafsiri ushuhuda wa Mungu. Kwa Upendo, Mungu alitoa ufunuo maalum kumhusu ili kutusaidia kupata majibu juu ya maswali hayo. Kupitia Agano la Kale na Agano Jipya, amejifunua kwetu, amejidhihirisha pasipo kuacha swali juu ya tabia yake ya upendo. Awali ufunuo ulikuja kupitia manabii, bali ufunuo wake kamili ulitufikia kupitia Yesu Kristo (Ebr.1:1-2). Biblia inayo matamko kuhusu ukweli ulioko kwa Mung una kumdhihirisha Mungu kama nafsi. Mafunuo yote ni muhimu. Twahitaji kumjua Mungu kupitia Yesu Kristo (Yoh.17:3) na ukweli ulio katika Yesu (Efe.4:21). Kupitia maandiko, Mungu anavunja vizuizi vya kiakili, kimauti na kiroho, akiwasilisha hamu yake kubwa kutuokoa.
2.0. LENGO LA MAANDIKO MATAKATIFU.

- Biblia humfunua Mungu na kumweka wazi Mwanadamu.
- Huweka wazi matatizo yetu na namna ya kuyatatua.
- Hutuwasilisha kuwa ni walipotea, tuliokosana na Mung una humfunua Yesu kuwa ndiye anayetutafutana kurudisha kwa Mungu. Na Yesu Kristo ndio lengo la Maandiko Matakatifu. Kwani Agano la Kale linaeleza kwamba mwana wa Mungu ni masihi, Mkombozi wa Ulimwengu na Agano Jipya linamfunua Yesu Kristo kuwa ni mwokozi.